Pages

Saturday, March 2, 2013

FILAMU YA "WAVES OF SORROW" YA MSANII RAY YAZINDULIWA KWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA VIZIWI



Nguli wa filamu bongo Vicent Kigosi “Ray”ameendeleza utamaduni wake wa kuzindua filamu kwa staili ya kutoa msaada na safari hii amezindua filamu ya Waves of Sorrow.


Ray alikeleka zawadi katika shule ya viziwi iliyopo Buguruni Malapa, akiambatana na wasanii walioshiriki katika filamu hiyo na kufurahi na watoto hao kwa kuwagawia zawadi mbalimbali.

Ray amekuwa akifanya hivyo kila anapotoa filamu mpya kutembelea vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu au wale wenye matatizo ya kiafya.


Ray alifunguka akieleza sababu inayo mfanya kuzindua filamu zake kwa mtindo huu “Nimefurahi kuwa pamoja na watoto hawa na kuwapatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao, mara nimekuwa nikifanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa mashabiki wa kazi zangu,wakati wengine wakila na kusaza pia kuna watu hawezi kufanya hivyonami kidogo nilicho nacho nagawana na watoto, yatima ambao wana matatizo mbalimbali ikiwa ni kutoa mchango katika kuwapa moyo,”