skip to main |
skip to sidebar
"HAZIPITI SIKU MBILI BILA KULIZWA NA KERO ZA WAANDISHI WA HABARI:.....MAMA KANUMBA
Mama yake mzazi na marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.
Akiongea na kipindi cha The Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.
“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.
Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku