Polisi wa Afrika Kusini bado wanaendelea kuchunguza tukio la kutisha linalodaiwa kufanywa na kijana wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 28 ambae anatuhumiwa kumuua bibi wa kizungu mwenye umri wa miaka 67 huko Johannesburg.
Bibi kizee Jette Jacobs ambae ni raia wa Australia alisafiri mpaka Johannesburg kwa lengo la kufunga ndoa na mwanaume anayempenda lakini siku mbili baada ya kukutana na mwanaume huyo, bibi huyo amekutwa amefariki kwenye mazingira ya kutatanisha kwenye jiji hilo lililo kwenye list ya majiji hatari kwa uhalifu duniani.
Mwili wa bibi huyu mwenye watoto sita ulikutwa kwenye guest house miezi miwili baada ya kuwasili Afrika Kusini ambapo kwa muda waliofahamiana online, Jette alikua ameshatuma kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili kwa Omokoh na mwanaume mwingine aitwae Isaac.
Pamoja na kupewa onyo na familia yake, Jette hakusikia chochote bali alitaka kwenda South Africa toka november 2012 ili akafunge ndoa na huyu mwanaume wa Kinigeria, kwenye guest house mwili wake ulipokutwa kuna baadhi ya vitu alivyokuwa navyo havijaonekana kama vile mikufu na pesa.
Binti wa mwisho wa bibi huyu amesema mwanaume huyu wa Nigeria alitaka kuhamia Australia ili akaishi na Bibi huyu lakini bibi aligoma na kumwambia anataka kwenda kuishi nae Nigeria.