Star wa muziki kutoka Kenya, maarufu kama Nonini "Mgenge True" ambae kwa sasa ni mtangazaji wa kituo cha redio, 1 FM[KE] amechaguliwa kuwa mmoja wa Member Of The Board Of Directors katika chombo kinachojihusisha na kusimamia na kufuatilia haki za wasanii nchini Kenya (PRISK).
Hivi karibuni, Nonini alitangazwa kuwa yeye ndiye msanii pekee kutoka nchini humo alieingiza kiasi kikubwa cha hela kutokana na muziki wake, baada ya kuchaguliwa kuwakilisha wasanii katika nafasi hiyo alizungumza hivi “I wanna take this opportunity to thank all the artist’s who came out for the PRISK (Performing Rights Organisation Of Kenya) Special AGM today and actually voted MgengeTrue into the Board of Directors! Artists should be involved in running copyright bodies because hakuna mtu anaelewa shida za msanii kama msanii! ”.
Pia wengine waliochaguliwa kuwakilisha wasanii katika bodi hiyo ni aliekuwa jaji Tusker Project Fame, Judge Ian.