Pages

Tuesday, March 5, 2013

Uchaguzi Mkuu Kenya: Uhuru Kenyatta Aongoza Dhidi Ya Raila Odinga...


Ikiwa bado uchaguzi unaendelea katika sehemu tofauti za nchini humo, haya ni matokeo ya awali ya uchaguzi Mkuunchini Kenya yanayoonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, Mtoto wa Raisi wa kwanza wa nchi hiyo Bw. Jomo Kenyatta [R.I.P], ndiye anaeongoza matokeo hayo kwa kura 1,621,410 ambayo ni sawa na asilimia (54.78%).
Huku akifuatiwa na aliewahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ndugu Raila Odinga ambae nae ana jumla ya kura1,203,802 ambazo ni sawa na jumla ya asilimia (40.67%). Namba hizi bado zinazidi kuongezeka kutoka katika vituo vya kuhesabia kura. Matokeo hayo ni kutoka katika vituo zaidi ya 8,300 kati 31,000 vilivyokuwa registered as poll stations.