Pages

Friday, March 8, 2013

Kijana Mwenye Umri Wa Miaka 19 Aliyeshinda Udiwani Nchini Kenya...


Ikiwa bado nchi ya Kenya ipo katika shauku kubwa ya kutaka kujua ni nani atakayeibuka mshindi na kuchukua madaraka ya kuongoza nchi hiyo ikiwa hadi sasa Uhuru Kenyatta (TNA) bado anaongoza kwa kura 4,835,482ambazo ni sawa na asilimia [49.5%] huku Raila Odinga (ODM) akiongoza kwa kura 4,316,005 ambazo ni sawa na asilimia [44.2%] lakini huyu ni kijana anaefahamika kwa jina la Kibiwott Munge ameshinda na kuwa diwani nchini humo.
Munge mwenye umri wa miaka 19 amefanikiwa kupata madaraka ya kuwa diwani na kuwashinda wagombea wengine ambao wana umri mkubwa ikwa sawa na baba yake.
Kijana huyo ambae alimaliza elimu yake ya form 4 mwaka jana na mwaka huu kuamua kujiingiza kwenye maswala ya siasa na kubahatika kuchukua uwadhifa huo wa udiwani.
Hii ni video inayoonesha mengi zaidi kuhusiana na yeye na nini kilichomsukuma hadi kuamua kujiingiza kwenye maswala ya kisiasa akiwa na umri mdogo: