Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.
Akilisimulia hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.
Aliongeza kuwa, ilifika mahali baadhi ya abiria walitaka kuwafungukia ukweli kwamba wanachokifanya si adabu hasa ikizingatiwa kuwa wao wana majina makubwa katika burudani za Bongo.
Kufuatia taarifa hizo na kudakwa kwa picha zao, Amani liliwasaka watuhumiwa hao kila mmoja kwa wakati wake ili kusikia kutoka kwao juu ya kufanya madudu ndani ya ‘pipa’.
“Jamani kwani mabusu yana shida gani, yule (Q-Chillah) ni mwanamuziki mwenzangu na tumezoeana. Yale yalikuwa ni mambo ya kawaida tu na utani, si vinginevyo,” alisema Shilole.
Q-Chillah simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokelewa, lakini baadhi ya watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo hana kawaida ya kupokea simu kama namba hazijui.