Pages

Saturday, April 6, 2013

WANASAYANSI WAGUNDUA KIFAA CHA KUSOMA NDOTO WANAZOOTA WATU USIKU



Wanasayansi nchini Japan jana wamesema wamepata njia ya kusoma ndoto za watu kwa kutumia scanner za MRI kugundua siri za fikira zisizojitambua.



Watafiti wamefanikiwa kile wanachokisema ni “kifaa cha kwanza duniani kutafsiri ndoto za usiku, jambo ambalo limewasumbua wanasayansi kwa miaka mingi.

Katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Science, watafiti wa maabara ya ATR Computational Neuroscience ya mjini Kyoto, magharibi mwa Japan, walitumia scanner za za magnetic resonance imaging (MRI) kubainisha ni sehemu gani kwenye ubongo unaokuwa ukifanya kazi wakati mtu anapokuwa usingizini.

Wanasayansi hao kisha waliwaamsha waotaji na kuwauliza picha walizoziona, mchakato ambao ulirudiwa mara 200.
Majibu hayo yalilinganishwa na ramani za ubongo zilizotengenezwa na scanner za MRI na kisha walitengeneza database kulingana na majibu.


Katika majaribio yaliyofuata waliweza kubashiri picha zipi walizoziona watu waliojitolea na ambao walipata jibu la uhakika kwa asilimia 60. 

Timu yake kwa sasa inajaribu kubashiri mambo mengi ya ndoto yakiwemo harufu, rangi, mawazo na pia story nzima za ndoto za watu. Hata hivyo mtafiti mkuu wa maabara hiyo Yukiyasu Kamitani alikiri kuwa bado kuna safari ndefu mpaka waweze kuielewa ndoto nzima.

Utafiti huo ulitumia tu picha walizoona watu hao muda mfupi kabla hawajaamshwa ambapo katika uzingizi totoro ambapo mtu huwa na ndoto zaidi zimebaki kuwa fumbo.

“Bado kuna mambo mengi yasiyojulikana, “ alilimbia shirika la habari la AFP.