Pages

Thursday, April 4, 2013

HII NDO KAULI YA UCHUNGU ALIYOTOA ABSALOM KIBANDA BAADA YA KUTEKWA NA KUTOBOLEWA JICHO



 Kauli  hii  ameitoa  kupitia  ukurasa  wake  wa  facebook:

Si jambo rahisi kibinadamu ingawa kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Japo miye ndiye mwenye maumivu makali na machungu mwilini yanayotokana na majeraha na ulemavu niliotiwa, mke wangu kipenzi al maarufu Mama Joshua alikuwa pembeni mwangu wakati wote nikiwa kitandani hospitalini Dar es Salaam hadi Milipark Afrika Kusini. Pole sana Angela. 

Matendo yanasema zaidi kuliko maneno...umepita nyakati nyingi sana ngumu juu yangu tangu mwaka 2000 tulipokutana na kuwa marafiki na hatimaye mwili mmoja. 

Ni Mungu tu atakayekulipa kile kinachostahili na si mwanadam