skip to main |
skip to sidebar
SAKATA LA MTOTO ALIYELAZIMISHWA KULA MBEGU ZA KIUME
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa), amefanyiwa unyama wa kutisha na baba yake wa kambo kwa kunajisiwa, kulawitiwa na kulazimishwa kulamba mbegu zake za kiume.
Mtoto huyo anayeishi mkoani Pwani, imedaiwa ana hali mbaya kiafya kutokana na kudaiwa kufanyiwa kitendo hicho kwa muda wa miaka miwili.
Mwanaume anayedaiwa kufanya unyama huo amefahamika kwa jina la Adam Taliani maarufu kama `Kiredio' (37).
Inadaiwa kuwa baba huyo alikuwa akifanya kitendo hicho mbele ya mama wa mtoto huyo ambaye ni mke wake, akiwatishia kuwaua kwa panga kama watatoa siri hiyo.
Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa mtoto huyo Chiku Selemani alisema vitendo hivyo alianza kufanyiwa na baba yake wa kambo tangu mwaka 2011 wakati mama yake alipoanza kuishi na mwanaume huyo.
Alisema, waligundua unyama huo baada ya mtoto huyo kuanza kusema kwa majirani zao jinsi baba yake anavyomfanyia vitendo hivyo usiku huku mama yake akishuhudia.
"Hapo mwanzo tulikuwa tunasikia kwa majirani kuwa mtoto wetu anasimulia mambo mazito, hata hivyo hatukumuamini sana," alisema Chiku.
Chiku alisema kitu ambacho kinamsikitisha kuona dada yake ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa akishuhudia jambo hilo na wakati mwingine walikuwa wakiingiliwa kwa zamu yeye na mtoto wake.
GIZA LA UNYAMA
Akisimulia huku akimwaga machozi, mtoto huyo ameliambia NIPASHE kuwa baba yake alianza kumuingilia wakati walipohamia kijiji cha Soga, Wilaya ya Kibaha mwaka 2011.
Alisema siku moja usiku wakati amelala, alimuona baba yake akimshika na kumlazimisha kumuingilia huku akimtisha kumkata kwa panga endapo atapiga kelele.
Alisema, aliogopa sana, alimuacha baba yake afanye anavyotaka na hapo ndipo ukawa mlolongo wa kufanyiwa unyama huo kila siku.
"Anaponiingilia napata maumivu makali, nataka kupiga kelele lakini naogopa ataniua kwa panga," alisema mtoto huyo.
Mtoto huyo alizidi kusema kwamba kwa kuhofia kuendelea kufanyiwa vitendo hivyo, aliamua kutoroka nyumbani kwao kila siku nyakati za jioni na kwenda kwa majirani, lakini wazazi wake walimtafuta na kumrudisha nyumbani.
Kutokana na kutoroka mara kwa mara, uongozi wa kijiji hicho uliamua kuwafukuza kijijini hapo na walirudi Mwandege mwishoni mwa mwaka huo.
"Tuliporudi baba alizidi kuniingilia, sasa ilikuwa anafanya kwa zamu, akitoka kwa mama anakuja kwangu na kuniingilia sehemu zote za siri," aliongeza kusema.
MAMA ASAIDIA KUEPUSHA KUNYIMWA UGALI
Hata hivyo alisema wakati anafanyiwa matukio hayo, mama yake anakuwa akishuhudia, wakati mwingine anamsihi asikatae anapoingiliwa kwa sababu watakosa chakula.
"Kila kitu ninachofanyiwa mama anakiona, nipapokataa mama ananiambia nisifanye hivyo ili tuendelee kula ugali wa baba," alisema mtoto huyo.
Alisema kutokana na kufanyiwa vitendo hivyo anaona sehemu zake za siri zimeharibika kwa vidonda.
ALAZIMISHWA KULA MBEGU ZA KIUME
Katika jambo la kusikitisha zaidi, mtoto huyo kabla na baada ya kuingiliwa hulazimishwa kula mbegu za kiume za baba yake ili kumsafisha.
Alisema, wakati baba yake anapomaliza kufanya mapenzi na mama yake, humfuata na kumwambia alambe mbegu zote, kisha anamuingilia mtoto huyo na anapomaliza humlazimisha tena kumsafisha kwa kumlamba.
NDUGU WAINGILIA KATI
Mama mdogo wa mtoto huyo, Chiku alisema baada ya kupata taarifa hizo, walilifikisha suala hilo ngazi ya ofisi ya kitongoji, kijiji na kituo cha polisi kwa ajili ya kumsaidia.
Alisema kwa kushirikiana na polisi wa kituo hicho, alifanikiwa kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Temeke, ambapo huko ilibainika mtoto huyo ameathirika na magonjwa ya zinaa.
Chiku alisema kwenye vipimo hivyo, iligundulika tumbo lake limejaa uchafu na alipatiwa huduma ya kumuondoa uchafu.
"Walinishauri kutokana na afya ya mtoto kuwa mbaya, nimpeleke hospitali ya karibu ya Mkuranga, huko atapewa huduma zote kulingana na magonjwa aliyokuwa nayo," alisema.
Alisema kutokana na kuwa peke yake katika suala hilo, hakuweza kuendelea nalo na badala yake aliliacha na kuendelea kuishi na mtoto huyo katika hali ngumu.
Chiku alisema hawezi kumlaumu sana dada yake, kwa sababu ana matatizo ya akili, ndio maana mwanaume huyo anaweza kufanikisha mambo yake bila kizuizi.
Alisema kutokana na maisha magumu anayoishi, hawezi kushughulikia tatizo hilo na mtuhumiwa kuchukuliwa hatua, aliomba watu binafsi mashirika mbalimbali ya haki za binadamu kuingilia kati.
Pamoja na hayo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, Urich Matei, alipoulizwa suala hilo, alisema bado hajalipata, akamuomba mwandishi asubiri ufafanuzi baada ya kupata taarifa kutoka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga.
"Taarifa hiyo sijaipata, ni mpya kwangu nakuomba niwaulize wenzangu wa Mkuranga na baadae nitakupatia ufafanuzi," alisema Kamanda Matei.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwandege Ally Ubuguyu alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alithibitisha kutokea.
Ubuguyu alisema baada kupata taarifa hizo, wametoa taarifa katika kituo cha Polisi Vikindu, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.
"Mtuhumiwa bado yupo hapa kijijini, lakini hakuna polisi aliyekuja kumkamata pamoja na kutaarifu juu ya tukio hili," alisema.
Alisema uongozi wake upo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa Polisi watakaokwenda kumkamata mtuhumiwa huyo, kwani kitendo alichokifanya ni kibaya.