skip to main |
skip to sidebar
BEYONCE, RIHANNA WACHANWA KUTUMIA CD JUKWAANI
Kutokana na msanii Ne -Yo kutoa maoni yake makali juu ya baadhi ya wasanii wanaoimba kwa kutumia CD maswali mengi yameibuka juu ya kuendelea kwa urafiki uliokuwepo katia yake na RihanaShtuma hizo zimewakumba waimbaji mahili wa kike Beyonce na Rihanna kuimba kwa kutumia CD kenye stage na ndipo alipoulizwa Ne- Yo swahili hilo alijibu kuwa " kama msanii unatakiwa kujua vyote yaani kuimba na kucheza ila unapotumia CD unaonyesha dhahiri uwezo wako mdogo hivyo kama mshabiki alikuwa anataka kusikiliza sauti yako angenunua CD na kusikilizia nyumbani hakukuwa na ulazima wa kufanya shoo " Ne Yo aliliambia gazeti la Daily Telegraph