Pages

Sunday, February 17, 2013

JUX NDANI YA PENZI ZITO NA JACKIE CLIFF


Unamkumbuka Jux? Yule chorus Killa wa kundi la Wakacha wazee wa  Coders? Yeah, jamaa yuko kimya kiaina lakini kwa mujibu wa picha zake za Instagram the boy is living large! Pamba kali (kama kawaida yake), trip za pipa za hapa na pale kwenda ughaibuni na mambo kibao.


Kikubwa zaidi the songbird is apparently dating one of the hottest  models in Tanzania, Jackie Cliff. Kama humfahamu vizuri Jackie  anaonekana kwenye video za nyimbo kadhaa za Bongo Flava zikiwemo Nataka  Kulewa wa Diamond na She got a gwan wa Ngwair!

Kupitia akaunti ya Instagram Jackie amepost picha akiwa na Jux na  kuandika, “Dinner date with @juma_jux in Garden hotel.”

Na pia Jux  kwenye akaunti yake amepost picha ya Jackie akijaribisha kuvaa viatu  vyake (Jux) na kuandika, “baby tryn them #me Jordans…#dope though.”