Pages

Sunday, February 10, 2013

Chris Brown Apata Ajali Ya Gari...

RnB singer kutoka Marekani anaetamba sana kwa sasa kwa uimbaji na kucheza kwake, Chris Brown amepata ajali ya gari jana huko Beverly Hills, Marekani.
Imeripotiwa kuwa, Breezy ambae alikuwa anaendesha gari yake aina ya Porsche kuelekea kwenye shughuli ya kujitolea alivamiwa na magari mawili ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakimfuatilia na ndio inasadikika wamesababisha ajali hiyo.
Paparazzi hao waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu na kutaka kumpiga picha ndio walisababisha gari ya mwanamuziki huyo kuharibika ingawa Chris Brown [ambae alikuwa mwenyewe kwenye gari] hakuumia popote.
Ona picha hapa chini: