Pages

Thursday, February 14, 2013

JACK PATRICK: NDOA YA MAMILIONI USALITI 100%

 

 
Na Hamida Hassan
MATENDO anayofanya mwanamitindo Jackline Patrick wakati mumewe Abdullatif Fundikira akiteseka gerezani, yametajwa kuwa ni usaliti wa asilimia miamoja na kwamba kama hatajirekebisha, mwisho wake utakuwa mbaya.

Jack akiwa beach na Martin Kadinda.
Hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni kupatikana kwa picha zinazomuonesha mwanadada huyo akiwa kimahaba zaidi na modo mwenzake wa kiume, Martin Kadinda.
Picha hizo zinawaonesha wawili hao wakiwa wamekumbatiana na kufanyiana mambo yasiyostahili kufanyika mbele za watu pale walipokuwa wakiogelea kwenye moja ya fukwe zilizopo jijini Dar na nyingine wakijiachia klabu.

J
ack akiwa kwenye pozi.
Wakizizungumzia picha hizo, baadhi ya wadau walioziona walisema kuwa, anachokifanya Jack si kizuri kwani ni usaliti wa dhahiri usiomfurahisha Mungu.
“Yule amefunga ndoa ya kifahari na Abdullatif, lakini leo hii mwenzake anateseka gerezani yeye anamsaliti huku uraiani, hii ni mbaya sana,” alisema Salim wa Mwananyamala jijini Dar.

Martin na Jack wakijiachia klabu.
Naye mama Oscar wa Kinondoni alihoji: “Huyu msichana anakosea sana kufanya haya tena hadharani. Hivi yule mume wake anayeteseka kule gerezani amemkosea nini mpaka anamfanyia usaliti wa wazi hivi?”
Jack akiwa klabu.
Mume wa Jack, Abdullatif Fundikira anayesota gerezani