Pages

Wednesday, February 6, 2013

Nicki Minaj anusurika kukamatwa mjini Dubai baada ya kumkumbatia polisi


Nicki Minaj anusurika kukamatwa mjini Dubai baada ya kumkumbatia polisi
Nicki Minaj amezungumzia jinsi alivyokaribia kukamatwa mjini Dubai kutokana na kumkumbatia ofisa wa polisi.
“Nilienda Dubai. Kidogo nijikute kwenye matatizo makubwa kwasababu wanaume wa Dubai  ni wazuri sana. Sitanii. Miongoni mwa sheria ni kwamba huwezi kumkumbatia mwanaume kama hajakuoa. Sasa wakati tunaondoka kulikuwa na mwanaume huyo ambaye alikuwa mzuri kweli, nikawa kama nasema ‘Bye!’ sababu nilitaka kuwa na wakati huu wa mwisho naye, “ Nicki alisimulia kwenye show ya Jimmy Kimmel. “Kumbe alikuwa polisi.”
Hawavai uniform za kipolisi. Ulikuwa kama uwanja wa ndege binafsi. Walikuwa wamevaa nguo za kawaida tu. Nilienda kumkumbatia na nilijikuta kama muda umesimama Dubai. Nilihisi kama kila kitu kiliganda.
Aliendelea:  Kila mtu kwenye timu yangu alidhani ntawekwa jela. Kilikuwa ni kitu cha kushtua. Alinyanyua mikono yake juu kidogo na kunipa tabasamu la woga na mimi nikawa kama samahani, samahani na nikaondoka.”