
Rapper maarufu kutoka nchini
Kenya,
CMB Prezzo ambae pia alikuwa ni mmoja wa washiriki wa
Big Brother Africa 2012 [StarGame] sasa anatarajia kufunga pingu za maisha na mwanadada ambae pia alishiriki shindano hilo mwaka huo huo,
Goldie Harvey ambae alikuwa ni mshiriki kutoka
Nigeria.
Prezzo alianza kujihusisha kimapenzi na
Goldie wakiwa katika jumba hilo ingawa hawakuonekana serious sana. Mara kadhaa
Goldie amekuwa akiulizwa na kukana mahusiano hayo hadi hivi karibuni iliporipotiwa kuwa
Prezzo alienda mjini
Lagos, Nigeria ambako inapoishi familia ya
Goldie na kwenda kutoa barua ya kutaka kumuoa.
Taarifa hizo zimetolewa na mtandao wa Big Brother na kusema kuwa wawili hao wamemua kufunga ndoa yao hiyo siku ya Jumapili ya tarehe 9 February mwaka huu mjini Lagos, Nigeria.