Pages

Wednesday, February 13, 2013

Msanii Kutoka Kundi La Wanaume Halisi Afariki Dunia Leo Asubuhi...


Kundi la Wanaume Halisi kutoka Temeke linalongozwa na msanii Juma Nature leo asubuhi limempoteza member mmoja wa kundi hilo anaefahamika kwa jina la Baraka Msale Sekera maarufu kama BK.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa na mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Rich One, amesema sababu za kifo cha marehemu BK ni alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya tumbo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa, jana alizidiwa na kupelekwa hospitali lakini hakufanikiwa kupona mpaka alipopoteza uhai asubuhi hii.