Pages

Tuesday, February 12, 2013

Nahreel Na Aika Wajitoa Pah One...

Kundi ambalo lilikuwa linaundwa wasanii wanne kwa pamoja likiitwa Pah One sasa limevunjika kwani First Lady wa kundi hilo la Pah One mwanadada Aika ametangaza kujitoa rasmi kwenye kundi hilo pamoja na rapper na producer wa kundi hilo Nahreel na hivyo kundi hilo kubakiwa na wasanii wawili tu.
Aika amesema kuwa sababu ya kumfanya ajitoe kwenye kundi hilo ni kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya kundi hilo na kuongeza kwa kusema Nahreel ni Solo Artist hivyo yeye na Nahreel hawajavunja kundi hilo na si kwamba mapenzi yake yeye na Nahreel ndiyo sababu iliyopelekea kuvunjika kwa kundi hilo.
Nahreel na Aika wanatarajia kuachia ngoma yao ya kwanza wakiwa kama Solo Artists tarehe 14 mwezi huu.