Timbulo msanii wa muziki na Filamu Swahiliwood.
Timbulo ambaye hivi sasa anatesa na wimbo wake wa Bado Kijana, tayari ameanza kazi ya upigaji picha wa filamu kali nay a kusisimua iitwayo World of Benefit.

Timbulo akiwa na mwigizaji mahiri katika filamu Rose Ndauka moja ya scene za filamu hiyo

Ndani ya filamu hiyo msanii huyo anapambana na wakongwe wa tasnia hiyo ya filamu kama Mohamed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mama Mjata, Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka na Awadhi Saleh ambaye anakuja juu katika tasnia ya filamu kwa sasa.
“Nimepata bahati kufanya kazi na wasanii wakongwe, lakini pia nimepata bahati ya kusimamiwa na maproducer mahiri kama Selles Mapunda na Seleman Mkangara, hivyo naamini itakuwa kazi bora” alisema Timbulo.
Filamu ya World of Benefit imetayarishwa na mtayarishaji wa filamu Hamees Suba ‘Kemikali’ na inaongozwa na Selles Mapunda ‘Director of Directors’, akisaidiwa na Suleiman Mkangara ‘Striker’ kwa upande wa upigaji picha wapo wataalamu kutoka Bollywood chini ya kampuni ya Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam.
.
Watalaam chini ya Madirector Selles na Mkangara wakiwa makini kufuatilia filamu ya World of Benefit.

Timbulo akiwa na Rose kitandani katika filamu ya World of Benefit