Pages

Thursday, March 14, 2013

DREAMS DO COME TRUE!!! Izzo Bizness Afanikisha Kufanya Ngoma Moja Na Jay Moe...


Baada ya kupata bahati na kutimiza moja ndoto zake ambazo alikuwa akiomba kwa Mungu, ambapo alifanikiwa kurekodi au kufanya kazi na Producer mkongwe, Master J, rapper kutoka Mbeya City, Izzo Bizness azidi kufikia ndoto zake hasa baada ya kufanikisha ndoto yake nyingine, na hii ni kurekodi ngoma moja na legend wa Hip-Hop Bongo, JAY MOE... Izzo's dreams been coming true...
Izzo Bizness alifanya hivyo jana, baada ya kurekodi ngoma hiyo ikiwa na beat ya KTB huku vocals na mixing ikifanywa na Master J himself...
Wiki kadhaa huko nyuma, Izzo alifanikiwa kurekodi dundo lingine na Producer Master J ikiwa ni offer kutoka kwa producer huyo...
What else from Izzo... GOD IS GOOD!!! Tunaisubiri ngoma bro...