Pages

Tuesday, March 12, 2013

LULU ASEMA KWASASA HATOONEKANA KATIKA FILAMU...AWA MTU WA BIBILIA NA VITABU


Msanii wa filamu nchini elizabeth michael amesema kuwa kwa sasa hafikirii kufanya filamu badala yake ameamua kujikita katika maswala yake ya elimu na kwasasa amejipanga kwa mambo ya elimu tu.

Wakizungumza na thesuperstarstz mapema hii leo wadau wa filamu wameonyesha kumtaka lulu arudi na kuonyesha makali yake katika filamu ambapo wadau hao wameonyesha kumkumbuka sana msanii huyo mwenye makeke awapo mbele ya camera.

Msanii huyu kwasasa yupo mafichoni akijipanga na wadau na wapenzi wake wameonyesha dhahiri kumiss sana lulu hadi wengine kusema wanataka kumuona tu hata kwa kawaida kama kwenye filamu imeshindikana,thesuperstarstz imeongea na baadhi ya wadau wa filamu maeneo ya karikoo katika maduka ya kanda na kubaini kuwa watu wamem misss sana lulu kwani kwa dakika chache katika duka moja la kandamaeneo ya karikoo, thesuperstarstz imeshuhudia watu kibao wakija katika duka hilo na kuuliza kama lulu ameshatowa filamu mpya.

Baada ya kukutana na wadau hao thesuperstarstz ilibisha hodi katika nyumba anayoishi lulu kwa msaada wa msanii Mahsen Hawadhi Dk Cheni aliyetusaidia kumpata lulu tulipoonana na lulu tulimuuliza juu ya kukaa kwake kimya ambapo alisema Najua kama wadau wamenimiss ila ninawaomba wanivumilie kwasasa kwani bado sijakaa vizuri najipanga kwaajili ya mambo yangu ya kurudi shule kwani nimejifunza mengi sana na nimejipanga sana katika mambo yangu ya kielimu,Alisemasa lulu.
Kwasasa msaanii huyo ameonekana kuwa mtulivu sana kwani muda mwingi anaonekana kushika biblia na kusoma novo kitu ambacho kinafanya kila anayemjua lulu kushangazwa na staili hii ya maisha mapya ya lulu na kumshangaa lulu huyu si yule wa zamani,na kufanya watu wakiri kuwa mwanadada lulu kabadilika sana,thesuperstarstz inampongeza lulu kwakukumbuka na kuamua kurudi shule na kwakutulia na kujipanga tena kwani tunaamini bado anayo nafasi kubwa sana ya kubadili maisha yake.