Pages

Saturday, March 16, 2013

MONALISA MBALI YA KUWA MUIGIZAJI PIA NI MCHEZAJI WA NETBOOL




NIKIWA uwanjani ni mchezaji ninayefuata sheria zote za mchezo wa netboll nikiwa nje ya uwanja mimi ni msanii ambaye ninazingatia ubunifu na ubora wa kazi zangu hayo ni maneno aliyoyasema msanii wa filamu nchini Monalisa alipokutana na mwandishi wa habari hii hivi karibuni

Mbali na kuwa muigizaji wa filamu msanii huyo ambaye pia ni mchezaji mahiri wa mpira wa netboll ambapo alianza kucheza mchezo huo akiwa anasoma shule ya msingi na kufanikiwa kuendelea nao hadi alipofika sekondari

Aliweza kufanikiwa kucheza katika timu mbalimbali pamoja na kufika katika ngazi ya kimataifa, mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA alipokuwa kwenye ngazi za shule ya msingi na sekondari huku akichezea nafasi ya mfungaji GA

Alisitisha kucheza mchezo huo kwa muda mrefu baada ya kumaliza masomo yake shule ya sekondari kwa sababu ya kukosa timu ya kuchezea mpira huo na ndipo alipojiunga katika sanaa ya uigizaji mwaka 1998

Ingawa aliweza kukaa muda mrefu bila ya kushiriki katika mechi yoyote ile aliweka wazi kuwa aliamini kuna siku moja tena atarudi katika nafasi yake ya uchezaji na bado ataendelea kucheza mchezo huo

Monalisa aliweza kurudi tena katika mchezo huo baada ya kujiunga katika timu ya bongo movi inayojulikana kwa jila la 'waswahili' alijikuta akitimiza ndoto zake za kuendelea na mchezo huo baada ya kujiunga tena timu hiyo ambayo mpaka sasa ndio anayoichezea

Mbali na kuchezea timu hiyo pia anachezea timu ijulikanayo kwa jina la 'The Bize Queens' ambayo ni timu ya kampuni ya Business Times Limited (BTL) katika mashindano ya NSSF yanayoendelea katika Uwanja wa TCC, Chang'ombe

Alieleza kuwa tangu aanze kucheza mchezo wa netiboli hajawahi kuumia jeraha kubwa lililomfanya ajutie kuupenda mchezo huo ingawa alipata maumivu madogo madogo ambayo yeye anayaona ya kawaida katika mchezo wowote ule

"Niliumia vidole, ni kawaida tu na sijawahi kupata jeraha lolote lile ambalo lininisababisha nijisikie vibaya kucheza mchezo huo hivyo mpaka sasa bado nacheza na ninaufurahia mchezo huo" alisema Monalisa

Aliongezea kuwa "Nikiwa uwanjani mimi ni mchezaji na siweki hisia zozote za kujifanya ni muigizaji hivyo nafwata sheria zote za uchezji niwapo mahali hapo ila nikiwa sehemu ya uigizaji navaa uhusiaka wa muigizaji ninayetumia ubunifu wa hali ya juu"

Kundi la mambo hayo ndilo lilikuwa la kwanza kumtambulisha msanii huyo kwenye sanaa ya uigizaji huku jina la Monalisa likiwa likisikika katika masikio ya washabiki wengi kwa ajili ya umahili wa kuigiza aliokuwa anauonyesha msanii huyo

Mbali na umahili huo Monalisa ameweka wazi kuwa mama yake ndiye mtu wa kwanza kumshawishi na kumfwata katika fani hiyo huku akiwa anatamani kuwa kama mama yake katika uigizaji, mama huyo pia ni muigizaji aliyeanza kuigiza katika kundi hilo la Mambo hayo