Pages

Friday, March 8, 2013

MKE WA MTU AZIANIKA PICHA ZAKE ZA UCHI KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK...NI AIBU KUZIONA INASIKITISHA


Ama kwa hakika hivi sasa dunia ni kama haina tena hamu na sisi wanadamu kwani tumejikuta tukifanya mambo ambayo hata wanyama ni aghalabu sana kufanya.

Matukio ni mengi sana hata mengine hayafai kuandikwa hapa thesuperstars tz imekuwa ikipokea picha za uchi za wake za watu na waume za watu ambao hupigwa na mahawara zao kwa lengo la kutaka penzi au pesa na anapokosa huzivujisha picha hizo kwa vyombo vya habari.

Ila habari hii imenistua kidogo kwani  mwanamke huyu asiyekuwa na hata chembe ya aibu aliamua kuzitundika picha zake kwenye mtandao wa facebook kwa madai kuwa mumewe hayupo na wala hana mpango na facebook kwa hiyo hawezi kuziona picha hizo chafu na zinazotia kinyaa,ambazo zimeshuhudiwa na thesuperstarstz na kushindwa kuziweka hapa.

Kitu cha kujiuliza ni kwamba hata kama huyo mwanume haingii facebook inamaana hana marafiki au ndugu ambao wapo facebook wakamuambia anayoyafanya mkewe? na kitu kingine hadi mwanamke tena mke wa mtu ufikie kuweka picha kama hizo unatafuta nini wakati umeolewa je unataka kumuonyesha nani mwili wako na una muonyesha ili iweje wakati mume wako yupo.