Pages

Thursday, March 21, 2013



Louise na Martine Fokkens wakiwa kazini.

MAPACHA wenye umri wa miaka 70 nchini Amsterdam, Uholanzi, wameamua kustaafu kazi yao ya ukahaba baada ya kuifanya kwa miaka 50. Mapacha hao Louise na Martine Fokkens wameamua kustaafu baada ya umri kuwatupa mkono na kudai kuwa kwa sasa hawapati wateja. 

Louise na Martine wamelala na jumla ya wanaume takribani 355,000, kila mmoja akiwa amejivinjari na wastani wa wanaume 177,500 kwa kipindi cha miaka 50, ambapo kwa mwaka mmoja kila mmoja alikuwa analala na wanaume 3,550 sawa na wanaume 295 kwa mwezi na kwa siku wanaume 9.
Mapacha hao ambao wanadaiwa kuwa makahaba wenye umri mkubwa zaidi  jijini  Amsterdam, walianza kazi hiyo wakiwa na umri wa miaka 20. Mapacha hao ni wazazi wa watoto saba, Louise akiwa na watoto wanne, na Martine yeye ana watoto watatu.

 Mapacha hao ambao walikuwa wakipenda kuvaa sare ya nguo nyekundu walitoa Filamu ya simulizi za kweli iitwayo 'Meet the Fokkens' na wanatarajia kutoa kitabu kitakachoelezea safari yao katika biashara ya ngono.