Pages

Friday, March 8, 2013

ROSE NDAUKA ANASWA KWA MGANGA WA KIENYEJI...!


STAA wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amedaiwa kurogwa ili asifanikiwe na kupoteza mvuto kwa jamii.
Chanzo chetu makini kwa sharti la kuchorwa jina lake gazetini kilimtonya paparazi wetu kuwa, staa huyo mwenye sura yenye mvuto amerogwa na wasanii wenzake ambao hawapendi mafanikio yake na ndiyo maana anakosa dili nyingi za kushuti kama zamani.
“Mara kwa mara amekuwa akipewa taarifa za kurogwa lakini yeye amekuwa akizipotezea sasa shauri yake, atapotea,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo za kuwa anarogwa, Rose alisema yeye haamini ushirikina ila alikiri kupokea taarifa hizo kutoka Zanzibar lakini maisha yake amemuachia Mungu.
“Nimekuwa nikipuuza habari hizi kwani nimezisikia sana, juzi nilipigiwa simu na mtu mmoja aliyedai anaishi Zanzibar na kuniambia kuna msanii alikwenda kunimaliza kishirikina hivyo kama ninataka kupona nimfuate kisiwani humo lakini mimi sikwenda ingawa kidogo nimekosa amani,” alisema Rose.