Pages

Sunday, March 31, 2013

JACK WOLPER AJIPANGA KUMUENZI KANUMBA


STAA wa  Bongo Movies, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa anatarajia kumuenzi marehemu kwa kuachia vipande vya filamu ya After Death ambayo ni mwendelezo wa filamu ambayo ilichezwa na marehemu Steven Kanumba, Uncle JJ.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Wolper alibainisha kuwa anatarajia kuonesha vipande vya filamu hiyo katika siku ya Kumbukumbu ya Kanumba itakayofanyika Aprili 7, mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

 “Ni filamu ambayo nimeiandaa katika mazingira maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba ambaye kila Mtanzania anatambua mchango wake kwenye sanaa,” alisema Wolper.

Coming Soon: Kaa Tayari Kwa Video Ya KIDELA Kutoka Kwa AbduKiba..

Msanii wa kizazi kipya, AbduKiba ambaye anatamba na baadhi ya ngoma zake kama Kizungu Zungu, Hatuna Habari Nao na hii ya sasa ambayo amemshirikisha AliKiba inayoitwa Kidela yuko tayari kuachia video yake mpya.

Abdu sasa yuko mbioni kuachia video ya wimbo wake wa Kidela aliyomshirikisha kaka yake Ali...
Video hiyo ambayo inafanyiwa shooting na Director Adam Juma kutoka Visual Lab/ Next Level. Hivyo kama wewe ni shabiki mkubwa wa AbduKiba basi kaa tayari kwa kichupa hicho ambacho kitadondoka soon..

Brand New: Chege ft. Malaika - USWAZI TAKE AWAY...

Ni video ya ngoma mpya ya Chege Chigunda "Mtoto Wa Mama Saidi" ikijulikana kama USWAZI TAKE AWAY...
Ni ngoma mpya na ya mwisho kuitoa ya Chege inayofanya vizuri sana kwa sasa akiwa amemshirikisha mwanadada MALAIKA katika Chorus na Bridge...
Video imefanywa na Director Adam Juma kutoka VISUAL LAB: NEXT LEVEL
Ndani ya video hii ameonekana Madee [MANZESE], Bibi Cheka pamoja na Mh. Temba katika kumpa tafu mkali mwenzao from TMK Wanaume Family...
Check zigo hapa chini:

PICHA: Mama Yeyoo Video Sound In The Making...

Its a photo inayomuonesha Ben Pol akiwa na Director Nisher wakifanya video ya MAMA YEYOO...
Gnako, Ben Pol na Nisher wako Arusha ku-shoot video ya ngoma hiyo..

HUYU NDO BINTI ALIYECHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA MPENZI WAKE BAADA YA KUBUSU KIFUA CHA DIAMOND JANA

Dada Huyu Akiwa kwenye show ya Diamond alinyanyuka na kwenda kubusu kifua cha diamond,baada ya hapo alichezeya kichapo toka kwa jamaa yake baada ya kujisikia vibaya na hicho kitendo...



Binti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya matiti Diamond Binti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya matiti Diamond

Binti huyo akilia baada ya kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake

Binti huyo akilia baada ya kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake
 
Binti alipokua kwenye show ya Diamond, uzalendo ulimshinda, akaenda kunyonya chuchu za diamond kama inavyoonekana pichani  Kitendo hicho kilimuudhi bwana wake, ambapo alimvuta binti huyo na kumchapa makofi. Katika picha ya pili, binti huyo anaonekana akilia baada ya kuchezea kichapo, huku akiwa amewekwa “chemba” na boyfriend wake.

MAUNO YA AUNT LULU YASABABISHA NJEMA IZIMIE


Njemba ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, amenusurika kifo kufuatia kuanguka ghafla na kupoteza fahamu kwa madai ya kuchanganywa na mauno ya Aunty Lulu

Mkasa huo ulijiri kwenye sherehe ndogo ya watu wa karibu baada ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na Gardner Dibibi, Kinondoni, Dar es Salaam wiki iliyopita.





Ilikuwa ni wakati wa ndugu, jamaa na marafiki wakipata msosi sanjari na vinywaji huku muziki ukipigwa nyumbani kwa familia ya bibi harusi, Kinondoni, ndipo Aunty Lulu alipoanza kukata mauno na kushangiliwa.


Wakati watu wakimpa dole Aunty Lulu, jamaa huyo alimtolea macho pima na kuanza kuchanganyikiwa na mauno hayo.


Polepole jamaa, mkono mmoja ukiwa umeshika sahani yenye msosi mwingine soda, aliganda kwa sekunde kadhaa kama vile haamini anachokiona.


Kufumba na kufumbua, njemba alikwenda chini ghafla na kupoteza fahamu.


Hali ya hewa ilichafuka kuanzia hapo, ikawa patashika nguo kuchanika.


Hata hivyo, wanaume majasiri waliokuwa eneo la tukio walimpepea jamaa huyo ambapo baadaye alizinduka. 

  
Jamaa huyo baada ya kurejewa na fahamu alisikika akisema: Ukweli wowowo la huyu dada (Aunty Lulu) limenichanganya, nusu linitoe roho jamani.


Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kilichomtokea jamaa huyo ni mfadhaiko

"MI NAJITUMA KWA BIDII..Q-CHIEF ANAKAA NA KUVUTA BANGI HALAFU ANADAI NATUMIA NYOTA YAKE....NAOMBA ANIKOME"...DIAMOND

Hii  ni  kauli  ya  msanii Diamond kuhusu Q chief: mi nafanya kazi, mazoezi na dancers, nahangaika kutafuta sare, kuandika nyimbo nzuri, wakati nafanya yote hayo we unakula unga, halafu unakuja kusema nasafiria nyota yako, nisafirie nyota ya mla unga? mi staki, staki, agombane na wakubwa wenzake kina dully mi aniache na wadogo wenzangu staki...?

LADY JAYDEE ADAI KUWA CLOUDS FM NI WANAFIKI....WANATAKA WAHONGWE ILI WAPIGE NYIMBO ZA WASANII


Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira"

"Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"

Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

"Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"

" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"

Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa

TAHADHARI KWA WANAOPENDA KUNUNUA "MALAYA"......DODOMA WAMENASWA WAKIWA NA ARVAs


WANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).


Kukamatwa kwa wanawake hao ambao ni Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na Ziada Mukamurera (25), kunafuatia mmoja wao Esperance kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kuwa alikuwa ameibiwa fedha taslimu Sh 800,000 na hati ya kusafiria.


Lakini, Polisi walipofika nyumba ya kulala wageni waliyofikia iliyopo eneo la Area D walikuta wanawake wengine wawili ambao walikuwa wakikaa chumba kimoja na Esperance.


Uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa mwanamke huyo hakuibiwa na kubaini wote si raia wa Tanzania. Hata hivyo kilikosekana kifungu cha kuwashitaki ndipo waliamua kupeleka sakata hilo Uhamiaji ili liweze kushughulikiwa.


Kulingana na maelezo yao, Esperance alitangulia kuja nchini kisha kuwaita wenzake ambao ilikuwa ni mara ya kwanza kuja nchini, lakini hata hivyo alisema kuwa, kumekuwa na makundi ya wanawake kutoka Rwanda wanaokuja nchini kipindi cha Bunge na hata mwaka jana kuna kundi lilikuja wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Uhamiaji, wanawake hao waliingia nchini na kujitambulisha kuwa walikuja Dodoma kufanya biashara ya vitenge, lakini hawakuwa hata na kitenge kimoja ambacho kingeweza kuwaonesha kuwa walikuwa wakifanya biashara hiyo.


Juhudi hizo za Uhamiaji zinadaiwa kuwafikisha hadi klabu moja maarufu ya usiku iliyopo eneo la Area D ambapo walinzi wa Kimasai walikiri kuwafahamu wanawake hao na walikuwa wakiwafuata nyumba ya wageni waliyofikia kama mtu alikuwa akiwahitaji na walikuwa na ni wateja wa klabu hiyo ya usiku.


Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Norah Massawe alikiri kukamatwa kwa wanawake hao na polisi na kukabidhiwa Uhamiaji.


Alisema mwanzoni wanawake hao walidai kuwa walikuja Dodoma kwa ajili ya kununua vitenge kwa ajili ya biashara na waliposhikiliwa na Polisi kwa siku kadhaa waliomba kurudishwa nchini kwao.


Alisema wawili kati yao walikutwa wakiwa na vidonge vya ARVs, lakini haijafahamika moja kwa moja kama walikuwa wagonjwa au la.


“Siwezi kusema walikuwa ni makahaba bali wanahisiwa hivyo kutokana na biashara waliyosema wanafanya kutoeleweka na hata maelezo ya walinzi wa klabu ya usiku kuwa walitambuliwa kama wateja wao, kwa kweli hilo siwezi kulithibitisha,” alisema.


Aliwataka wananchi kuwa makini na watu wasiowafahamu kwani hivi sasa Mkoa wa Dodoma umekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu hasa katika kipindi cha Bunge.


Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Dodoma, Audrey Njelekela ambaye alisema kuwa, wamekuwa wakitoa elimu kuanzia ngazi ya Mkoa hadi mtaa ambapo kuna timu ya Mkoa ya Ukimwi na hata kwenye halmashauri kuna waratibu ambao wamekuwa akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Ukimwi.


Alisema kuwa kwa sasa kiwango cha maambukizi kwa Mkoa wa Dodoma ni asilimia 2.9 kwa takwimu za mwaka 2011 na 2012 ikilinganisha na takwimu za mwaka 2007 hadi 2008 ambapo kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 3.3.


Alisema kuwa waratibu wa ngazi ya halmashauri wamekuwa wakitoa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi kwenye maendeleo mbalimbali ikiwemo klabu za usiku.


Alisema kwa kuwa kondomu zinasambazwa maeneo mbalimbali yakiwemo ya starehe ni vyema wananchi kuhakikisha wanazitumia. “Matumizi ya kondomu ni muhimu sana kwani maeneo ya klabu za usiku na maeneo mengine ya starehe watu wengi wanachukuana tu lakini wanakuwa hawafahamiani,“ alisema.


Alisema kuwa kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu katika Mkoa wa Dodoma hasa kipindi cha Bunge, umakini zaidi unahitajika.

HIZI NDO PICHA ZA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI- ZANZIBAR


 Hapo ndio tujue kuwa wenzetu hawabahatishi na hawana siasa kwenye kazi zao proffessional....kazi kweli kweli!!wamehadithiwa tu wamemchora mtu yule yule!!Angalia Mchoro wa Polisi Hapo chini na Ufananishe na mtu Huyu..


Mchoro Uliyotumika Kumpata Muuaji

SUGU APINGA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE KUITWA "JAKAYA KIKWETE"


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) amesema haungi mkono pendekezo la Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema mapendekezo hayo yametolewa na watu wenye kutaka kujipendekeza kwa mkuu wa nchi badala ya kufikiria kuutangaza Mkoa wa Mbeya katika nyanja ya kimataifa.


Alisema Mbeya ina historia ya kutaka kujitangaza kimataifa na uwanja huo ni fursa pekee ya kufikia malengo hayo aliyoeleza kuwa yanataka kufifishwa na wateule wa rais.


“Siungi mkono uwanja kuitwa kwa jina la JK, tunataka jina litakaloasisi uhalisia wa Mbeya nasi tufahamike kimataifa, kamati ya ushauri ya mkoa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Norman Sigala ilikurupuka kuleta wazo hilo kabla ya kuwasiliana na wabunge,” alisema.


Alisema hatua hiyo ya Sigala haiwakilishi mawazo ya wananchi bali inawakilisha mawazo ya mtu aliyeteuliwa na kwamba wao wakiwa wawakilishi wa Mkoa wa Mbeya kwa ridhaa ya wananchi hawawezi kukubaliana na suala hilo.


Kauli ya Sugu iliungwa mkono na wabunge wengine wa Mkoa wa Mbeya, ambapo Mchungaji Lukson Mwanjale wa Mbeya Vijijini (CCM) alisema anasikitishwa na hatua hiyo ya kuliwasilisha wazo hilo bila ya kuwashirikisha wabunge.


Alisema wakati wa kikao cha kamati ya ushauri wabunge wengi hawakuwepo na taarifa hizo walizisikia baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari.


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo ambaye pia ni mbunge wa Songwe, aliomba apewe muda wa kutaka kujua sababu zilizoibua wazo hilo.


Wazo la kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete linazidi kupata upinzani ambapo awali chama cha NCCR-Mageuzi na kile cha PPT Maendeleo kupitia kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya vilipinga wazo hilo.

Thursday, March 28, 2013

Hemedy PHD Asema "BORA KUOA"... "NABADILISHA NUMBER"...


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambae pia ni mcheza filamu hodari hapa BongoHemedy PHD jana aliandika kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema BORA KUOA...
Ni nini kilichomkuta PHD?? Well PHD aliandika hayo kutokana na usumbufu mkubwa anaoonekana kuupata kutoka kwa watu katika simu yake ya mkononi...
Hemedy (@hemedyPHD) ambae alilalamika kuwa amechoka na kuwa-block simu/watu hawa lakini pia kufikia kuona bora aoe alitweet " Nimeshindwa kuhandle pressure ya wasumbufu ktk simu yangu! Maisha ya kublock simu pia nimechoka! BORA KUOA! sijui itasaidia?? NABADILISHA NUMBER"
Hemedy aliandika haya huku ikonekana wanaomsumbua zaidi ni wasichana/wanawake ambapo amefikiria ni bora aoe ili kupunguza au kuondoa usumbufu huu...
Pamoja na mawazo haya, pia PHD (Star wa single GOING CRAZY) amejiuliza kama hili litasaidia kuondokana na usumbufu huu anaoupata sasa...
Hemedy amekuwa akiongelea mara kwa mara kuhusu yeye kupendwa na wasichana ambayo may be ni muonekano au kazi zake za kisanii anazofanya...
PHD pia aliwahi kusema kuwa siku akiamua kuoa inabidi aandae shindano la kutafuta mke bora (kama ilivyo katika kusaka vipaji) ambae ataishi nae milele ili kumpata yule anaefaa..

Nisher Akabiliwa Na Kazi Kubwa...


Director mkali wa video kutoka Arusha, Nisher from NISHER ENT. ameona kuwa na kazi kubwa ya videos inayomkabili....
Nisher (@NISHER_) ambae ashafanya video nzuri na kutokea kupendwa sana, i.e. LISTEN by Belle 9, PRESS PLAY by DJ Choka, DOLE by Mabeste n.k. ameyasema haya baada ya kuanza kupata simu mbali mbali kutoka kwa stars tofauti, ikiwemo wale ambao walishawahi fanya video zao zamani na kuhitaji zirudiwe...
Stars hao ambao ambao wamekuwa wakihitaji kazi zao zirudiwe na nyingi zikiwa za zamani lakini zikifanya vizuri radioni mpaka leo wanaonekana kumtafuta Nisher ili kufanya kitu kizuri zaidi...
Nisher alionesha kuona kazi kubwa inayomkabili kutoka kwa stars hawa ingawa kuna mpya ambazo pia atahitaji kuzifanya...
Good to notice this bruh, Go do your thing!!... Great videos is all we need... BIG UP!!

COMING SOON: Darassa ft. Ditto - Milele...


Baada ya kufanya vizuri na baadhi ya track zake zikiwemo Sikati Tamaa pamoja na Nishike Mkono, sasa rapperDarassa yuko mbioni kuachia ngoma yake nyingine mpya ambayo inakwenda kwa jina la ''MILELE''.
Darassa anatarajia kuiachia ngoma hiyo hivi karibuni ambapo ndani ya ngoma hiyo amemshirikisha mwanamuziki kutokaTHT maarufu kama Ditto.
Pia ngoma hii ni moja kati ya ngoma ambazo zitakuwepo katika album yake ya Sikati Tamaa.

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO....


HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO....

..
.
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..
..

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAMMPONGEZA WEMA SEPETU



SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limempongeza msanii wa kike Wema Sepetu kwa moyo wa upendo aliouonyesha kwa msanii mwenzie Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya sh. milioni 13 alizotozwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kupatikana na hatia katika kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wengine rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema kuwa imani na moyo wa upendo aliokuwa nao msanii Wema ndio uliomsukuma kumlipia kiwango hicho cha fedha bila ya kujiuliza mara mbili kitendo hiko kimeonyesha jinsi gani wanavyohitaji kushirikiana katika matatizo

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujifunza kutoka kwake kwani wanahitaji kuwa kitu kimoja kujaliana kwenye matatizo na kutambua kuwa wao ni familia moja wanaojenga nyumba moja

"Kitendo alichoonyesha msanii mwenzetu ni kitendo cha kuigwa na cha kiimani siyo kwamba anauwezo sana hapana ila kujali na utu ndio kilichomsukuma atoe fedha hizo" alisema Mwakifwamba

"Unajua kuwa nacho na kutoa ni vitu tofauti wengi pale walikuwa navyo ila labada hawakuwa na moyo wa kutoa hivyo Wema mungu atambariki na kumuongezea pale alipopunguza " aliongeza Mwakifamba

Mwakifamba alimtaka Kajala kutoa shukurani kwa mungu kwa kumsaidia kumtoa kule alipokuwa kwani sehemu yenye mateso na inayoumiza katika maisha ya kila siku

Wakati huo huo kwa upande wake Msanii Wema Sepetu "Imenichukua masaa mawili kufanikisha hili,nilienda benki nikatoa fedha na kuja hapa kulipa, ni sh.milioni 13".Hii ni kauli ya Msanii wa Filamu Wema Sepetu akizungumza na waandishi wa habari buda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kumlipia faini ya kiasi hicho cha fedha msanii mwenzake Kajala Masanja.

Wema alisema kuwa mumlipia Kajala kiasi hicho cha fedha haoni kama amepoteza kwani msanii huyo ni kama ndugu yake wa karibu.

"Katika vitu vingi sana,kumsaidia kwangu sijaona kama nimepoteza chochote,naona kama nimetoa kitu kama mtu  yoyote anayeweza kufanya hivi kwasababu kutoa ni moyo,sihitaji kulipwa chochote mwenyezimungu ndiye atanilipia"alisema

Aliongeza kuwa "Nahakika hakuna mtu anayependa kukaa gerezani,kwahiyo nimeona kama nitafanya hivyo nitamuokoa katika hali zote mbaya"

Kwaupande wake Dkt.Cheni alimewataka wasanii nchini kuwa na ushirikiano pale mmoja wao anapopatwa na matatizo kwani wao ni kitu kimoja na ni familia moja hivyo kushirikiana kwao ndio kutaendelea kuimalisha undugu walio nao na kufanikiwa katika kazi wanayoikusudia

Alisema katika maisha hakuna mtu aliyewekwa alama usoni kuwa atakuwa wa matatizi tu bali kila mtu anaweza kupata tatizo kwa aina yoyote hivyo tunatakiwa tuwe karibu.

"Kiukweli sina la kusema zaidi kwani matatizo yanamkuta kila mtu na yanapokukuta unakuwa haujajua,Mtu unaweza kuona unafanya jambo sahihihi lakini kijamii au kisheria linakuwa tatizo,ninachoomba kwa wasanii wenzangu tuwe na ushirikiano pale mwenzetu anapopatwa na tatizo kama hili tujitoe kwa mwenzetu"Alisema Dkt.Cheni.

Awali Dk.Cheni alisema kuwa wangeweza kuchangishana kiasi hicho cha fedha na kuzilipa lakini baadaye Wema alionekana akitoka mbio katika viwanja vya mahakama hiyo na kwenda katika gari lake ambapo ilidaiwa alikwenda benki kutoa fedha.

Kajala alitoka gerezani baada ya kulipiwa kiasi hicho cha fedha na msanii mwenzake Wema Sepetu muda mfupi baada ya kusomwa hukumu hiyo.

BINTI WA MIAKA 16 ALAZIMISHWA KUNYWA MKOJO NA MAMA YAKE MDOGO HUKO IRINGA



Vituko mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16 mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.

Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi  kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa mshindo.

Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na kuingia ndani na  ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake  mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake  mdogo.

Katika kipigo hicho Zawadi  alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.

Zawadi inadaiwa aliwahi kwenda zanzibar kwa nia ya kufanya kazi na baada ya muda mama yake mzazi ambaye jina lake bado halijafahamika alimpigia simu arudi nyumbani na mara baada ya kurudi ndipo kutokuelewana huko kukajitokeza.

Aidha taarifa za ndani kuhusu tukio hilo zinasema kuwa Mama yake Msichana Zawadi alitupwa akiwa mchanga na kuokotwa na wasamalia wema na hatimaye kulelewa na Bibi yake ambaye hata hivyo amefariki duni.

Kisa cha yote hayo ni madai ya mtoto zawadi kuomba aoneshwe Baba yake mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazo zipata kutoka kwa ushirika wa ndugu zake hao.Zawadi pamoja na majirani wameuambia mtandao huu kuwa vitu vilivyo tumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za simu,mkandaa,na vipande vya chupa katika kumchoma navyo.

Hata hivyo hadi mtandao huu unachapisha taarifa hii watuhumiwa wa tukio hili yaani Mama mzazi pamoja na Mama mdogo wa Zawadi wanashikiliwa na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia kwa mahojiano zaidi.

"NILIWAHI MFUMA SINTAH AKIJIUZA MAENEO YA MANZESE"...RAYUU



Katika  kile  kinachoonekana  kuwa  ni  mwendelezo  wa  ugomvi  wa Sintah  na Rayuu, wasanii  hawa  wameendelea  kurushiana  matusi  ya  nguoni  na  kuumbuana  kila  siku......

Sintah aliwahi  mtuhumu  Rayuu  kuwa  ni  kahaba  mwenye  kiwango  na  aliyeshindikana.Tuhuma  hizo  zilikuja  baada  ya picha  za uchi za msanii Rayuu  kuvuja  mtandaoni  zikionesha  makalio  na  matiti  yake.....

Baada  ya  tuhumu  hizo, Rayuu  naye  ameendelea  kufichua  mambo  mengi  kuhusiana na Sintah kwa  kudai  kuwa  Sintah  ni  kahaba  na  haoni  aibu  maana  umri  wake  umeenda....

Rayuu  anadai  kuwa  ukahaba  ulimfanya  Sintah aachwe  na Juma  Nature.Msanii  huyu  ameenda  mbali  zaidi  baada  ya  kudai  kuwa  amewahi  muona  Sintah  kwa  macho  yake  akijiuza  maeneo  ya  Manzese.....

Hiyo  ni  post  ya  Rayuu aliyoitupia  facebook  jana.

MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET ATIWA MBARONI



MENEJA wa Wafanyakazi wa Ndani ya Ndege wa Kampuni ya Fastjet Emma Donovan, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kujibu shtaka linalomkabili la kutoa lugha ya matusi.

Emma (40) alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Joyce Minde.
Katuga alidai Machi 19 mwaka huu Emma alimtolea lugha ya matusi Samson Itinde jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Emma alikana shtaka hilo ambapo Katuga alidai upelelezi umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe kwa usikilizwaji wa awali.

Hakimu Joyce alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi lakini kwa kuzingatia vigezo vya dhamana vitakavyotolewa kwa kuwa mshtakiwa ni raia wa kigeni.

Alitaja masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria au kutoa fedha taslim sh milioni tano na pia awe na wadhamini wawili ambao ni Watanzania.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 ili kupangwa tarehe ya kuanza kwa usikilizwaji wa awali

MACHANGUDOA WAJIUZA MBELE YA NYUMBA YA WAZIRI MKUU....



Issa Mnally na Richard Bukos-GPL
KWELI ni aibu kwa taifa kama la Tanzania, lenye ulinzi uliotimia lakini ni ajabu sana kuwaona wanawake wanaoishi mjini kwa kutegemea biashara haramu ya kuuza miili ‘machangudoa’ wamefikia kuifanya jirani kabisa na makazi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda.

Wiki iliyopita, waandishi  wetu  waliwanasa machangudoa hao wakiwa wanazurura kwenye Barabara ya Kenyatta inayopita mbele ya makazi ya waziri mkuu takriban mita 80 kutoka barabarani kwa lengo la kujiuza.


Ili kulijua hilo kwa undani, waandshi wetu walijifanya wateja kabla ya kuwapiga picha ili kuweza kuzungumza nao mawili matatu kuhusu kuwepo eneo hilo lenye heshima zake.
Mmoja wa ‘wauza sukari’ hao aliyejitambulisha kwa jina la Hawa, mkazi wa Kinondoni, alikiri yeye na wenzake kufanya biashara hiyo kwenye eneo hilo.


“Ni kweli mimi na wenzangu tunapiga kambi eneo hili, huwa ikifika usiku tunaanzia kule Coco halafu tunakuja hadi huku, lakini mbona maswali mengi, unataka tufanye biashara kama vipi sepa,” alisema changu huyo akianza kupandisha jazba.


Kikubwa walichokiongea machangu hao walisema barabara hiyo yote hupitwa na viongozi wakubwa na wafanyabishara ambao baadhi yao ni wateja wao wakubwa. Wakasema hawamwamini sana mteja anayekwenda na Bajaj au Bodaboda kwa vile wanasumbua kutafuta eneo la kufanyia ngono.


“Wateja wetu wengi ni wale tunaomalizana ndani ya gari, hawa wa Bajaj na Bodaboda wengi wanataka kwenye majani, ni rahisi kukamatwa na polisi wa doria,” 
alisema changudoa mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Suzy lakini hakuwa tayari kutaja yaliko makazi yake.

Inakuwaje wauza miili hao watanue eneo ambalo kimazingira linapitiwa na viongozi mbalimbali wazito kama vile mabalozi wa nje waliopo Tanzania, mawaziri, akiwemo waziri mkuu mwenyewe ambaye ni jirani kabisa na makazi yake?

Yapo madai kwamba, askari wanaovalia mavazi ya kiraia ambao wanapaswa kuhakikisha usalama wa eneo lote la Coco Beach wanakaushia matendo hayo kwa kile kinachodaiwa wanapozwa na kitu kidogo.


“Askari wapo, lakini sema baadhi yao wanatufahamu, kwa hiyo ikitokea na sisi mambo yetu yamekaa vizuri tunachekiana,” alisema Suzy.